VIRUTUBISHI,MAKUNDI YA VYAKULA NA MLO KAMILI Utangulizi: Chakula ni muhimu kwa binadamu wote. Chakula huupatia mwili virutubishi mbalimbali kwa ajili ya kuuwezesha kufanya kazi mbalimbali. Ili kuwa na hali nzuri ya lishe ni vyema kuzingatia ulaji unaofaa ikiwa ni pamoja na mlo kamili. Ulaji unaofaa ni muhimu kwa watu wote. Ulishaji unaofaa kwa watoto kulingana na umri ni muhimu hasa kwa ukuaji na maendeleo yao. Maana ya maneno yanayotumika katika masuala ya lishe Chakula ni kitu chochote kinacholiwa na kuupatia mwili virutubishi mbalimbali. Chakula huupatia mwili nguvu, kuulinda na kuukinga dhidi ya maradhi mbalimbali. Mfano wa chakula ni ugali, wali, maharagwe, ndizi, viazi, mchicha, nyama, samaki, matunda n.k. Lishe ni mchakato unaohusisha hatua mbalimbali za jinsi mwili unavyokitumia chakula kilicholiwa. Hatua hizi ni kuanzia chakula kinapoliwa, jinsi mwili unavyokisaga na kukiyeyusha, umetaboli na hatimaye virutubishi kufyonzwa na kutumika mwilini. Virutubish i...
Comments
Post a Comment