Skip to main content

Kizazi cha milenia



Kizazi cha milenia : Je ni kweli wao ndio kizazi kisichokuwa na bahati zaidi duniani?


Millennialst,

Vijana wa kizazi kipya, kwa kweli, wana uwezekano mkubwa wa kuwa na deni kuliko mababu zao


Walikuwa kizazi cha kwanza kuishi na kompyuta za kibinafsi, simu za rununu, mtandao na kupata mtiririko wa habari kutoka utotoni.


Walikuwa na matarajio makubwa juu yao wenyewe: na miaka mingi zaidi ya elimu kuhusiana na wazazi wao na muundo tofauti zaidi wa kijamii, kizazi cha milenia (watu waliozaliwa kati ya 1981 na 1996) yaani vijana wa kizazi kipya walioota kuwa na mafanikio zaidi na mabadiliko ya kiulimwengu kuliko vizazi vingi vya awali.


Hata hivyo, uchunguzi wa kimataifa unaonyesha kuwa milenia au vijana wa kizazi kipya, kwa kweli, wana uwezekano mkubwa wa kuwa na deni kuliko mababu zao na kuchukua muda mrefu, kwa wastani, kuondoka nyumbani kwa wazazi wao au kufikia hatua za kitamaduni za maisha ya watu wazima, kama vile kununua mali au gari.



Kutengana huku kati ya matarajio na ukweli, kumefanya vijana hawa wa milenia kuwa shabaha ya picha za mizaha mitandaoni yaani 'memes' na maoni ya dharau kwenye mitandao ya kijamii juu ya "kutofaulu" kwao, "uvivu" na utegemezi mkubwa kwa wazazi wao.


Kibaya zaidi, sasa wanakejeliwa kwa dharau na kizazi cha Z, kile kinachorithi milenia, ambao kwa jumla wanachukulia kizazi cha milenia kama "kisichofaa".


Hivyo basi, ni nini kilikoseka kwa milenia - na je! Ni kweli wamefeli?


'Kulaumiwa isivyo haki'

Jibu kutoka kwa watafiti wengi, kwanza kabisa, lawama sio haswa kwa kizazi hiki.


Illustration showing a man approaching a door ajar

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

'Kizazi kisichokuwa na bahati zaidi katika historia'


"Milenia wamekuwa watu wazima katika siku za mwanzo za simu za mkononi na nyakati za kuungana", Jason Dorsey, rais wa Kituo cha Generational Kinecticism (kampuni inayofanya utafiti juu ya tabia za vizazi vya milenia na Z ulimwenguni), amearifu BBC.


"Kwa hivyo, kwa namna fulani, walikuwa mahali pazuri kwa wakati unaofaa, kuja na maoni mazuri juu ya jukumu lao ulimwenguni".


"Wazazi wao waliwaambia watafaulu, walikuwa na ufikiaji mpana wa elimu ikilinganishwa na vizazi vilivyopita, na kulikuwa na hisia ya juu ya uunganisho na ushawishi fulani. "


'Kizazi kisichokuwa na bahati zaidi katika historia'

Lakini Dorsey anasema kuwa milenia wamelazimika kukabiliwa na changamoto kubwa kama vile kuzorota kwa uchumi kulikofuatia mgogoro wa kifedha wa mwaka 2008 hadi 2009 na hivi karibuni janga la Covid-19.


"Kwa njia nyingi, kizazi cha milenia kilikuwa kipo katika nafasi ya kuwa na mafanikio makubwa sana, lakini walikumbana na aina fulani ya kuzorota kwa uchumi, huku wengi wao wakiachishwa kazi, kutokea kwa mfumko wa bei na kupanda kwa gharama ya maisha", Dorsey anaendelea kusema.


Hoja ya mtaalam pia inaungwa mkono na takwimu ya data.

Kizazi cha milenia kitabeba makovu ya uchumi huu katika kipindi chao chote cha maisha, kulingana na Dorsey


Nchini Marekani, nakala ya gazeti la Washington Post, Juni 2020, ilitaja milenia kama "kizazi kisicho na bahati katika historia ya Marekani.


"Kwa kuzingatia mgogoro wa sasa (janga la Covid-19), kizazi cha milenia kwa wastani, kimeshuhudia ukuaji wa uchumi wa polepole tangu kuingia kwenye soko la ajira kuliko kizazi kingine chochote katika historia ya nchi", makala hiyo ilisoma.


"Kizazi cha milenia kitabeba makovu ya uchumi huu katika kipindi chao chote cha maisha, kama mfumo wa mapato ya chini, ustawi wa chini na kupiga hatua za maisha kuchelewa kama umiliki wa nyumba."


Hatua zilizopigwa na kila kizazi

Bila shaka, kila kizazi kinakabiliwa na changamoto za aina yake na ndio kile Dorsey anachokiita "nyakati muhimu" - matukio yanayoashiria kizazi kwa njia ambazo zinaathiri uwoga wao, elimu na machaguo katika maisha yao, maadili, na maoni ya siku zijazo.


Kizazi "kimya" yaani "silent" (kilichozaliwa kati ya 1928 na 1945), kwa mfano, kilitambulika pakubwa na Vita vya Pili vya Dunia.


Kizazi cha Baby boomers (1946-64) walikumbana na matukio ya kiulimwengu kama vile Vita vya Vietnam au kuwasili kwa mtu kwenda kwenye mwezi kwa mara ya kwanza.


Kizazi X (1965-1980), ambacho kilikuja baadaye, kilishuhudia kumalizika kwa Vita Baridi na kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Ukimwi yaani VVU.


Kizazi Z (watu waliozaliwa kati ya 1997 na 2012), kwa upande wake, hakika wataathiriwa sana na ujio wa janga la Covid-19.


"Hadi kuwasili kwa kizazi cha Z, milenia walikuwa kizazi sawa zaidi (kwa kila mmoja) ulimwenguni",

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

"Hadi kuwasili kwa kizazi cha Z, milenia walikuwa kizazi sawa zaidi (kwa kila mmoja) ulimwenguni"


Vizazi vyote vinaweza pia kuathiriwa na matukio makubwa ya mahali, kama vile majanga ya asili, magonjwa ya milipuko au matukio ya kisiasa yenye kufadhaisha.


Kwa hivyo, nini kinachotenga kizazi cha milenia?

Hoja kuu, anasema Jason Dorsey, ni kupanda kwa gharama kubwa ya maisha (haswa katika elimu na kwenye miji mingi ulimwenguni hasa gharama ya nyumba au makazi) na kuongezea kwa kiwango cha kufikia matukio ya kiulimwengu ambayo hayangekuwa na matokeo makubwa, ikiwa hatungeishi katika ulimwengu unaotuunganisha.


"Hadi kuwasili kwa kizazi cha Z, milenia walikuwa kizazi sawa zaidi (kwa kila mmoja) ulimwenguni", anasema.


"Je! Hii inamaanisha kuwa watu ni sawa?


Hapana.


Lakini inamaanisha wana kufanana kwingi katika kile wanachofikiria juu ya mawasiliano, burudani, utamaduni na kushiriki katika siasa."


"Uchumi umeunganika zaidi, kama vile mifumo ya benki na usambazaji. Na, ikiwa tunaangalia kazi, waajiri wengi wakubwa ni wa kimataifa."


"Kizazi kina hisia ya uunganisho ambayo haikuwepo hapo awali", anaongeza mtaalam.


Dorsey anaelezea kuwa milenia wanajua mengi kuhusu matukio ya ulimwengu kwasababu ya mtiririko wa habari na unganisho, ambako kulibadilisha matukio ya kawaida tu kuwa ya kiulimwengu.


CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kizazi cha milenia kimekua na kina aina tofauti sana ya mkataba wa mwajiri na mwajiriwa


"Kizungumzii juu ya matukio kama vita vya ulimwengu, lakini wazo kwamba mgogoro wa benki katika nchi moja kunaweza kuwa na athari kubwa kwa wengine na kuenea ulimwenguni kote.


"Hiyo ni muhimu sana."


'Uchumi wa pamoja' na ukosefu wa usalama katika ajira

Kwa kuongezea, milenia wanakabiliwa na ukosefu wa usalama katika ajira zaidi kuliko kizazi cha wazazi wao kwa ujumla.


Marekebisho ya kifedha, kubadilika kwa sheria za kazi, ushindani katika soko la ajira na maendeleo ya uchumi wa pamoja ni baadhi ya mazingira ambayo hufanya kizazi cha milenia kuwa na maisha ya kitaalam ambayo wakati mwingine ni rahisi kubadilika na wazi kwa ubunifu - lakini pia wakati mwingine haina uhakika na hukumbwa na hatari nyingi.


"Kizazi cha milenia kimekua na kina aina tofauti sana ya mkataba wa mwajiri na mwajiriwa kuliko kizazi kilichopita", anaelezea Dorsey.


"Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa hawakutarajia kufanya kazi katika kampuni moja maisha yao yote, au kuwa na mwajiri mmoja kwa maisha yao yote".


Mtaalam anaelezea kuwa hii ilisababisha hisia ya msisimko na uhuru - wazo kwamba "ninaweza kuanzisha kazi au taaluma yangu mwenyewe".


Lakini kuna upande mwingine wa shilingi.


"Waajiri huenda hawawezi kutoa faida sawa kama vile bima ya afya. Jukumu linaishia kuhama kutoka kwa mwajiri kwenda milenia", Dorsey anasema.


CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kizazi cha milenia kinakabiliwa na changamoto ya kupata ajira kuliko wazazi wao'


"Sina majibu, lakini ni ubunifu ambao una pande nzuri na hasi, na hasi zinaathiri kizazi kimoja zaidi ya kingine", anaongeza.


Ni changamoto ambayo husababisha kizazi cha milenia kujisikia kuchanganyikiwa, kulingana na maoni ya Dorsey.


"Walishtushwa na changamoto hizi ambazo ziliwalazimisha kuweka kando vitu vingi: kuchelewesha taaluma zao, ndoa yao, kupata watoto, kununua nyumba na hata kuweka akiba itakayomsaidia akistaafu".


"Kizazi cha milenia kilianza kuhisi kuwa malengo mengi waliyojiwekea yalikandamizwa. Na hata wale wenye bahati zaidi ambao waliendelea kufanya kazi na kusonga mbele kimaisha, walihisi kwamba kulikuwa na pingamizi nyingi dhidi yao", anaendelea.


"Inaweza kusemwa kuwa kizazi hiki, wanahisi kuwa mambo hayafikiwi kwasababu zilizo nje ya uwezo wao zaidi kuliko vizazi vilivyopita."


Nguvu ya kizazi cha milenia

Lakini sio kwamba kila kitu ni giza kwa kizazi cha milenia.


Utafiti unaonyesha kuwa wako wazi zaidi kukubali utofauti na wanajua zaidi athari za tabia yao ya matumizi kuliko vizazi vilivyopita.


Kwa mfano, ni kizazi cha kwanza kuchukua hatua dhidi ya pengo la malipo kijinsia na kutafuta usawa wa ajira.


CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Lakini kizazi cha milenia kilikua watu wazima wakati ambapo mtandao uliweka wajasiriamali kwenye majukwaa ya mitandaoni"


Ingawa wataalam kama Dorsey wanaamini kuwa mabadiliko ya kina zaidi yanaweza kuachwa kwa kizazi Z. Milenia pia inathamini sana ujasiriamali - zaidi ya wazazi wao au babu na nyanya zao.


"Kilikuwa kizazi (cha kwanza) kuona wajasiriamali kama wenye kuvutia au washauri. Katika vizazi vingine, (msukumo) wa aina hiyo huenda ukachochewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni kubwa, wakuu wa serikali au washiriki wa majukumu mengine", Dorsey anaelezea.


Lakini kizazi cha milenia kilikua watu wazima wakati ambapo mtandao uliweka wajasiriamali kwenye majukwaa ya mitandaoni", anaelezea Dorsey.


"Kwa kuongezea, milenia inaweza kuanzisha biashara kwenye wavuti kwa gharama ya chini sana. Walakini, kile tulichoona ni kwamba milenia wengi walifungua biashara sambamba na kazi zingine (kama nyongeza ya mapato)."


Dorsey pia ameona katika utafiti wake idadi kubwa ya milenia wanafikiria tena chaguo za taaluma zao kutafuta mwelekeo mpya katika kazi zao - jambo ambalo halingewezekana kuzingatiwa na wazazi wao wengi wakati walipokuwa na umri huo.


"Pia kwasababu ya janga la corona, milenia wengi wanafikiria kwa kina juu ya kile kilicho muhimu kwao na jinsi wanavyotumia wakati wao."


CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

"Lakini sio kwamba kila kitu ni giza kwa kizazi cha milenia.," Dorsey anasema


Kwa jumla, Dorsey anasema, yeye na watafiti wenzake wa kizazi chake wana "matumaini makubwa juu ya kizazi cha milenia."


"Milenia wana ustadi mzuri, ni kizazi kichanga na kitafaidika na ahueni yoyote ile ya kiuchumi itakayojitokeza katika miaka michache ijayo", anasema.


"Pia wana muda mwingi mbele yao kufanya maamuzi na kutimiza ndoto zao."


Mgawanyiko kati ya vizazi kutoka cha "silent" hadi Z

Huenda ikajitokeza kama mzaha lakini kwa watafiti, mgawanyiko huu ni muhimu sana.


CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

"Walitambulishwa kwa teknolojia mapema au baadaye''


"Ni nyenzo ya kuchambua mabadiliko katika maoni kadiri muda unavyokwenda", ameandika Michael Dimoch, rais wa kituo cha Pew, taasisi inayoongoza kwa utafiti Marekani.


"Hii ni njia kwetu kuelewa utofauti wa muundo mbalimbali (kama vile matukio ya ulimwengu na mabadiliko ya kiteknolojia, uchumi na kijamii) vinaingiliana na mzunguko wa maisha na kuzeeka ili kubadilisha maoni ya watu juu ya ulimwengu."


Dorsey anaelezea kuwa zaidi ya mwaka wa kwanza, kizazi hiki kinajieleza na kujiwekea malengo kupitia "mawasiliano yao ya kwanza na teknolojia, iwe wanaishi mijini au maeneo ya viungani na wazazi wao, kiwango cha na elimu na kipato chao" kwa sababu hiyo inaweza kuamua kama "walitambulishwa kwa teknolojia mapema au baadaye".



Comments

Popular posts from this blog

AirPods Fake Vs Real – How To Spot Fake AirPods In 2021 (Ultimate Guide)

AirPods Fake Vs Real – How To Spot Fake AirPods In 2021 (Ultimate Guide) Need your item authenticated by us? Proven expertise, not self-claimed. Get checked by the industry's top experts. Get Authenticated Want this item? Buy it from our partners! Looking to learn how to spot fake AirPods? Scared of getting scammed? Look no further, as we’ve compiled the most complete legit check guide for Apple AirPods. To put it shortly, the quickest way to spot fake AirPods is to scan the serial number found on the inside of the case (see pictures below on how to find that serial number). Once you get that code, pop it through  checkcoverage.apple.com  and see whether Apple confirms it for you. If you can’t get ahold of this code, we’ve added fake vs real comparisons for the actual AirPods below! Remember, fake AirPods will always compromise on quality. To highlight the most common places where these compromises are made, we’ve put together the comparisons you’ll find below. In this guide we'

Breaking news: Haji S. Manara ahamia yanga

  Aliekua msemaji mkuu wa Simba SC maarufu H. S. Manara. Baada ya kutokea kutokuelewana na klabu yake aliyokua akiitumikia, leo tar 24 August 2021 ametambulishwa rasmi Yanga SC na ya kusaini kandarasi akiwa kama msemaji huru.  Nimekiwekea baadhi ya matukio bofya kuangalia. Tujikumbushe pia enzi akiwa Simba SC. 

Aina ya sita ya vyakula ambavyo vikichanganywa hugeuka sumu

  Aina ya sita ya vyakula ambavyo vikichanganywa hugeuka sumu Kila binadamu ana kile alichojaaliwa na Mungu. Siku zote anachoamua mmoja kula huenda kikawa sumu kwa mwingine. Chakula anachokula mtu kinaenda sanjari na hali ya kiafya. Wengine huumwa hadi kusababisha kupoteza uhai na hii ni baada tu ya kupendelea kuchanganya chakula. Mtu mmoja anaweza kula sawa na kwa urahisi, ila kwa mwingine kikageuka sumu. Hali hii huchochewa zaidi na matokeo ya baadae pale unaposhindwa kuweka mchanganyiko sahihi na wenye afya zaidi . Kila aina chakula ina faida zake, ila kinapochanganywa kinaweza kusababisha shida kwa mtu. Kwa watu ambao wanataka kuchanganya lishe ili kupunguza unene na vichocheo vyake ni vyema kushauriana na wataalamu jinsi ya kupanga lishe bora. Mtaalam wa lishe wa Nigeria Habiba Haruna ameiambia BBC kuhusu aina sita za chakula ambazo zinaweza kuwa sumu kwa mtu yeyote. Samaki na Maziwa Samaki na Maziwa ni vyakula vyenye virutubisho lukuki na kuvichanganya katika sehemu moja vinaweza