Ilipoishia Simulizi : Kifo Siku Ya Harusi Yangu Sehemu Ya Kwanza (1) Baada ya kutambulishwa darasani, Farida akatokea kuwa rafiki mkubwa wa Genesis pamoja na kijana mwingine aitwaye Chris. Katika mazungumzo yao, Farida ambaye ameitingisha shule hiyo kwa uzuri wake, wavulana wakiwa wamepania kumpata, aligundua Genesis ni mtoto kutoka familia tofauti sana na yake kiuchumi lakini hakuwa na majivuno na alikuwa muungwana. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO. Huo ndio ulikuwa mwanzo, sumaku ya mapenzi ilionekana kuwavuta karibu kadri siku zilivyozidi kusonga ingawa wote wawili walipambana nayo. Mpaka umri huo wote walikuwa bikira, kama hivi ndivyo hata wanaume wanaweza kuitwa kama hawajakutana na mwanamke kimwili! Genesis tangu kuzaliwa kwake alikuwa bado hajamjua mwanamke, kwani aliamini kufanya hivyo ilikuwa ni dhambi kubwa ambayo mtu alistahili kuchomwa moto siku ya mwisho, hivyo ndivyo alivyofundishwa na wazazi wake na pia kanisani siku za Jumap...