Skip to main content

Simulizi : Kifo Siku Ya Harusi Yangu Sehemu Ya Pili (2)

 

Ilipoishia  Simulizi : Kifo Siku Ya Harusi Yangu Sehemu Ya Kwanza (1)

Baada ya kutambulishwa darasani, Farida akatokea kuwa rafiki mkubwa wa Genesis pamoja na kijana mwingine aitwaye Chris. Katika mazungumzo yao, Farida ambaye ameitingisha shule hiyo kwa uzuri wake, wavulana wakiwa wamepania kumpata, aligundua Genesis ni mtoto kutoka familia tofauti sana na yake kiuchumi lakini hakuwa na majivuno na alikuwa muungwana. 

 

Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO. 

 

Huo ndio ulikuwa mwanzo, sumaku ya mapenzi ilionekana kuwavuta karibu kadri siku zilivyozidi kusonga ingawa wote wawili walipambana nayo. Mpaka umri huo wote walikuwa bikira, kama hivi ndivyo hata wanaume wanaweza kuitwa kama hawajakutana na mwanamke kimwili! Genesis tangu kuzaliwa kwake alikuwa bado hajamjua mwanamke, kwani aliamini kufanya hivyo ilikuwa ni dhambi kubwa ambayo mtu alistahili kuchomwa moto siku ya mwisho, hivyo ndivyo alivyofundishwa na wazazi wake na pia kanisani siku za Jumapili. 

 

Ilikuwa hivyo pia kwa Farida, mtoto wa kiislamu aliyelelewa kwa maadili mema kila siku akiambiwa bikra yake ilikuwa zawadi kwa mume ambaye angemuoa na aliahidi kuitunza zawadi hiyo mpaka siku ya harusi. Alijitahidi kadri ya uwezo wake kupambana na vishawishi vyote vya wanaume aliokutana nao na kumtamani, kuanzia walimu mpaka wanafunzi wenzake. 

 

Sasa amekutana na Genesis ambaye kama ilivyotokea kwa kila msichana aliyemuona, Farida anajikuta moyoni akitamka neno “Whaoo!” kwa mshangao alioupata kutokana na mvuto wa Genesis, hana uhakika kama kweli ataweza kuyatunza maneno ya mama yake, miguu iliishiwa nguvu. 

 

Kwa Genesis pia ulikuwa ni mtafaruku kichwani mwake, hakukumbuka kama aliwahi kukutana na msichana mrembo kama Farida! Hakujali tena maneno ya wazazi wake ya kuangalia alikuwa na uhusiano na msichana kutoka familia gani, cha muhimu kwake ulikuwa ni uzuri na tabia ya msichana. Farida alimbadilisha kabisa, alikuwa na kila kitu ambacho mwanaume alikihitaji kutoka kwa mwanamke, kwamba familia yake ilikuwa maskini ya watu wasioelimika, halikuwa jambo muhimu kwake. 

 

“Haijalishi, cha muhimu kwangu ni uzuri na tabia ya mtu, digrii hazinisaidii kitu, labda akatae mwenyewe, akikubali sitamuacha!” Aliwaza Genesis, ilikuwa ni ghafla mno kufikiria yote hayo kwa sababu ndiyo kwanza walikuwa wamekutana, lakini alijikuta tu akiwaza na kufikia maamuzi hayo. 

 

Mioyo yao iliteseka mno lakini hakuwepo mtu jasiri wa kufungua mdomo kumweleza mwenzake hisia alizokuwa nazo moyoni mwake, waliishia kuahidiana tu “kesho nitamwambia” lakini haikuwa hivyo, Genesis hakuwa na uzoefu hata kidogo wa kutongoza, alichokifanya ni kuhakikisha maisha ya Farida shuleni yanakwenda vizuri, akishirikiana naye kwa kila kitu na hata kumpatia fedha za matumizi, kwa mwamvuli wa urafiki. 

 

Farida alielewa vizuri kilichoendelea moyoni mwa rafiki yake, kwani hicho ndicho pia kilichomsumbua yeye, lakini akiwa mwanamke asingeweza kuanza kumweleza mwanaume hisia zake za kimapenzi, haukuwa utamaduni wa Kiafrika. Akabaki kimya akisubiri siku ambayo Genesis angefungua mdomo na kumweleza, hiyo ndiyo ingekuwa siku ya furaha zaidi maishani mwake. 

 

Haikuwa hivyo, Genesis aliendelea kubaki kimya, yeye pia akitarajia Farida ndiye aanze kama ambavyo wasichana wengine waliwahi kumwita na kumweleza wazi walivyompenda, jambo ambalo kwa Farida lilikuwa haliwezekani, siku zikazidi kusonga hatimaye mwisho wa mwaka ukafika, shule zikafungwa na wote wakarejea jijini Dar es Salaam. Urafiki wao uliendelea, Genesis akimtembelea Farida nyumbani kwao kila mara na wazazi wake kumfurahia. 

 

“Jumatatu nitakuja nikuchukue twende nyumbani, ukawaone wazazi wangu!” 

 

“Sawa! Watafurahi kuniona?” 

 

“Mhhhh! Watafurahi” 

 

“Mbona umeitikia kwa shingo upande? Unanitisha” 

 

“Wala usitishike, Jumatatu nitakuja asubuhi nikuchukue tupite kwanza Kariakoo!” 

 

“Sawa!” 

 

Farida alibaki mwenye kusubiri kwa siku kadhaa mpaka siku hiyo ya Jumatatu ikafika, Genesis akafika akiwa na gari iliyoendeshwa na dereva wao mwanaume wa makamo. Baada ya kuwasalimia wazazi wa Farida, waliaga na kuondoka hadi Kariakoo mtaa wa Kongo, ambako katika hali ambayo hakuitarajia, Farida aliingizwa kwenye duka la nguo na kununuliwa nguo mpya pamoja na viatu. Zoezi hilo lililopokamilika ndipo waliondoka kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwao Genesis, maeneo ya Masaki karibu na hoteli ya GoldenTulip. 

 

Ilikuwa saa tano kamili walipofika, hawakumkuta mtu zaidi ya wafanyakazi, baba na mama tayari walishaondoka kwenda kazini. Farida hakuamini rafiki yake alitoka kwenye familia tajiri kiasi hicho, maishani mwake hakuwahi hata mara moja kuingia ndani ya nyumba iliyopambwa kiasi kile. Alipolinganisha na nyumbani kwao, ilikuwa ni sawa na usiku na mchana. 

 

“Hongera sana Genesis!” 

 

“Kwanini?” 

 

“Umebarikiwa!” 

 

“Kwanini unasema hivyo?” 

 

“Kupata wazazi wa aina yako ni bahati!” 

 

“Hata wewe pia umebarikiwa, hivi vitu ni vya kupita, cha muhimu ni upendo wa wazazi ambao wako tayari kufanya kila kitu kuhakikisha unafanikiwa maishani mwako, wazazi wako si wanakupenda?” 

 

“Sana!” 

 

“Basi hiyo inatosha, hata kama mnalala na njaa!” 

 

“Ahsante sana!” 

 

Walizungumza mengi wakiwa peke yao mpaka saa saba na nusu, miungurumo ya magari ikasikika nje ya nyumba, Genesis akanyanyuka kwenda kuchungulia dirishani na sauti yake ikasikika akisema “Dad and Mom are back!” Akimaanisha baba na mama wamerudi. Moyo wa Farida ukaingiwa na hofu na kuanza kupiga kwa kasi, akiuliza kama kulikuwa na mlango wa nyuma ili apate kutoka nje kisha kuondoka. 

 

“Kwanini?” 

 

“Naogopa!” 

 

“Nini?” 

 

“Wazazi wako!” 

 

“Kwa sababu gani?” 

 

“ Wanaweza wasinipende!” 

 

“Wewe unataka kupendwa na wazazi wangu au mimi?” 

 

“Wewe!” 

 

“Tulia basi!” 

 

Farida akarejea kwenye kiti na kutulia, haukupita muda mrefu sana kengele ikalia na Genesis akaenda kufungua mlango, wazazi wake wote wawili wakaingia wakiongozana na watu wengine wawili walioonekana kuwa mke na mume. Genesis na Farida wakawasalimia kisha wote wakaketi chini na maongezi kuendelea, wazazi wa Genesis wakionekana kama vile hawakumkuta mgeni mwingine sebuleni, hawakujali kabisa uwepo wa Farida. 

 

“Baba!” 

 

“Naam!” 

 

“Huyu hapa ni rafiki yangu, anaitwa Farida!” 

 

“Aaaaah! Karibu sana, anaishi wapi?” 

 

“Mikocheni!” 

 

“Hapana siyo Mikocheni, Mtoni kwa Aziz All…!”Farida alishindwa kumalizia sentensi yake baada ya kumuona Genesis akimkonyeza, alishachelewa. 

 

“Mtoni kwa Aziz Ally?” Baba yake Genesis aliuliza kwa mshangao. 

 

“Ndiyo!” Farida akaitikia, Genesis akiwa kimya. 

 

“Wazazi wako wanafanya kazi gani?” 

 

“Baba ni fundi selemara na mama ni mama lishe!” Aliongea Farida kwa kujiamini, kwake hapakuwa na tatizo lolote kwa sababu ni kazi ya wazazi wake na hakuona aibu, kwani kwake kazi ilikuwa ni heshima hata kama ni ndogo kiasi gani, hivyo ndivyo baba na mama yake walivyomwambia kila siku lililopokuja suala la kufanya kazi. 

 

 

 

“Genesis!” Baba yake aliita. 

 

“Naam baba!” 

 

“Hebu nendeni mkaongelee huko nyuma!” 

 

“Kwanini baba?” 

 

“Huyu ni Dk Rwegoshora, rafiki yangu wa siku nyingi, yuko na mke wake, kwa muda mrefu sana wameishi Uswisi lakini wamerejea nchini wiki iliyopita, ameteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, huyu ni binti yao anaitwa Bianca! Tupeni nafasi tuzungumze kidogo” 

 

 

 

“Sawa baba!” Genesis aliitikia akimnyanyua Farida kitini ili watoke nje, alishaelewa kila kitu kilichotokea, kusikia neno Mtoni kwa Aziz Ally kulimkera baba yake. Laiti kama Farida angeacha tu neno Mikocheni libaki, hakika wasingetolewa nje. Kwa unyonge wakatembea wakiufuata mlango, kisha kufungua na kutoka hadi kwenye nyumba nyingine iliyokuwa kando, wakaingia ndani ambako Farida alianza kulia, bila hata kuelezwa tayari alishajua kilichotokea. 

 

 

 

“Nilikuambia niondoke ukakataa, unaona sasa yaliyotokea?” Alisema maneno hayo, Genesis akimkumbatia. 

 

“Nisamehe!” 

 

Kwa usoni, Genesis Greyson Mshana, bwana harusi ambaye alikuwa anamuoa mtoto wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali aitwaye Bianca, alionekana mwenye furaha sana, lakini ndani yake alikuwa na mawazo mengi sana. Pamoja na kwamba alikuwa ndani ya suti na Bianca akimeremeta na shela, bado akili yake ilikuwa juu ya mpenzi wake Farida. 

 

Lakini akiwa katika mawazo ya machozi, ambayo tayari alishamweleza ukweli mkewe kuwa alikuwa anamuwaza sana Farida, simu yake ikaingiza ujumbe mfupi wa anuwani pepe na neno la siri ili akafungue, ambapo atakutana na siri nzito. 

 

Akamuomba mpambe wake Kelvin amwambie MC atangaze kwamba wanataka kwenda kupumzika, hilo likafanyika na wakatoka ukumbini. Kelvin na Martina wakawaacha chumbani, hapo ndipo alipoona kitu cha ajabu sana kwenye anuwani pepe ile. 

 

Uamuzi wake ulikuwa mmoja tu; kumuua Bianca kisha yeye mwenyewe kujiua. Hilo lilifanyika, akamchoma kisu Bianca na kuhakikisha kuwa kweli alikufa, kisha naye kupanda dirishani na kujirusha hadi chini, ili apasuke vipande vipande na kufariki! 

 

Kwanini aliamua kufanya mauaji hayo ya kikatili? Je, alipojirusha dirishani alikufa? 

 

Upande wa pili, Genesis anasimulia historia ya maisha yake, jinsi alivyokutana na Farida shuleni. Farida anatoka katika familia ya kimasikini sana, lakini ukaribu wao unaibua hisia nzito ambazo hakuna mmoja aliyekuwa tayari kufungua mdomo na kusema kinachoendelea moyoni mwake. 

 

Wakati wa likizo, Genesis alikuwa anakwenda kumtembelea Farida nyumbani kwao mara kwa mara, lakini siku Farida aliyokwenda nyumbani kwao na kujitambulisha kuwa anatoka Mtoni Kwa Aziz Ally, tena kwenye familia ya baba Fundi Seremala na mama Mama Ntilie, baba yake na Genesis akawaambia watoke nje, kwa kuwa walikuwa na mazungumzo muhimu na Bwana na Bibi Rwegoshora! 

 

Hiyo ilikuwa ishara ya kukataliwa! Genesis na Farida wakatoka kwa unyonge, huku Farida akilia kwa uchungu. 

 

Je, nini kitatokea?

Comments

Popular posts from this blog

AirPods Fake Vs Real – How To Spot Fake AirPods In 2021 (Ultimate Guide)

AirPods Fake Vs Real – How To Spot Fake AirPods In 2021 (Ultimate Guide) Need your item authenticated by us? Proven expertise, not self-claimed. Get checked by the industry's top experts. Get Authenticated Want this item? Buy it from our partners! Looking to learn how to spot fake AirPods? Scared of getting scammed? Look no further, as we’ve compiled the most complete legit check guide for Apple AirPods. To put it shortly, the quickest way to spot fake AirPods is to scan the serial number found on the inside of the case (see pictures below on how to find that serial number). Once you get that code, pop it through  checkcoverage.apple.com  and see whether Apple confirms it for you. If you can’t get ahold of this code, we’ve added fake vs real comparisons for the actual AirPods below! Remember, fake AirPods will always compromise on quality. To highlight the most common places where these compromises are made, we’ve put together the comparisons you’ll find below. In this gu...

Breaking news: Haji S. Manara ahamia yanga

  Aliekua msemaji mkuu wa Simba SC maarufu H. S. Manara. Baada ya kutokea kutokuelewana na klabu yake aliyokua akiitumikia, leo tar 24 August 2021 ametambulishwa rasmi Yanga SC na ya kusaini kandarasi akiwa kama msemaji huru.  Nimekiwekea baadhi ya matukio bofya kuangalia. Tujikumbushe pia enzi akiwa Simba SC. 

Aina ya sita ya vyakula ambavyo vikichanganywa hugeuka sumu

  Aina ya sita ya vyakula ambavyo vikichanganywa hugeuka sumu Kila binadamu ana kile alichojaaliwa na Mungu. Siku zote anachoamua mmoja kula huenda kikawa sumu kwa mwingine. Chakula anachokula mtu kinaenda sanjari na hali ya kiafya. Wengine huumwa hadi kusababisha kupoteza uhai na hii ni baada tu ya kupendelea kuchanganya chakula. Mtu mmoja anaweza kula sawa na kwa urahisi, ila kwa mwingine kikageuka sumu. Hali hii huchochewa zaidi na matokeo ya baadae pale unaposhindwa kuweka mchanganyiko sahihi na wenye afya zaidi . Kila aina chakula ina faida zake, ila kinapochanganywa kinaweza kusababisha shida kwa mtu. Kwa watu ambao wanataka kuchanganya lishe ili kupunguza unene na vichocheo vyake ni vyema kushauriana na wataalamu jinsi ya kupanga lishe bora. Mtaalam wa lishe wa Nigeria Habiba Haruna ameiambia BBC kuhusu aina sita za chakula ambazo zinaweza kuwa sumu kwa mtu yeyote. Samaki na Maziwa Samaki na Maziwa ni vyakula vyenye virutubisho lukuki na kuvichanganya katika sehemu moja vina...