Skip to main content

Simulizi : Kifo Siku Ya Harusi Yangu Sehemu Ya 3

 



Waweza kusoma sehemu zilizopita 

Simulizi : Kifo Siku Ya Harusi Yangu Sehemu Ya Kwanza (1)

Simulizi : Kifo Siku Ya Harusi Yangu Sehemu Ya pili (2)

SONGANAYO

Simulizi : Kifo Siku Ya Harusi Yangu Sehemu Ya 3

Kwa usoni, Genesis Greyson Mshana, bwana harusi ambaye alikuwa anamuoa mtoto wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali aitwaye Bianca, alionekana mwenye furaha sana, lakini ndani yake alikuwa na mawazo mengi sana. Pamoja na kwamba alikuwa ndani ya suti na Bianca akimeremeta na shela, bado akili yake ilikuwa juu ya mpenzi wake Farida.

Lakini akiwa katika mawazo ya machozi, ambayo tayari alishamweleza ukweli mkewe kuwa alikuwa anamuwaza sana Farida, simu yake ikaingiza ujumbe mfupi wa anuwani pepe na neno la siri ili akafungue, ambapo atakutana na siri nzito.

Akamuomba mpambe wake Kelvin amwambie MC atangaze kwamba wanataka kwenda kupumzika, hilo likafanyika na wakatoka ukumbini. Kelvin na Martina wakawaacha chumbani, hapo ndipo alipoona kitu cha ajabu sana kwenye anuwani pepe ile.

Uamuzi wake ulikuwa mmoja tu; kumuua Bianca kisha yeye mwenyewe kujiua. Hilo lilifanyika, akamchoma kisu Bianca na kuhakikisha kuwa kweli alikufa, kisha naye kupanda dirishani na kujirusha hadi chini, ili apasuke vipande vipande na kufariki!

Kwanini aliamua kufanya mauaji hayo ya kikatili? Je, alipojirusha dirishani alikufa?
Upande wa pili, Genesis anasimulia historia ya maisha yake, jinsi alivyokutana na Farida shuleni. Farida anatoka katika familia ya kimasikini sana, lakini ukaribu wao unaibua hisia nzito ambazo hakuna mmoja aliyekuwa tayari kufungua mdomo na kusema kinachoendelea moyoni mwake.

Wakati wa likizo, Genesis alikuwa anakwenda kumtembelea Farida nyumbani kwao mara kwa mara, lakini siku Farida aliyokwenda nyumbani kwao na kujitambulisha kuwa anatoka Mtoni Kwa Aziz Ally, tena kwenye familia ya baba Fundi Seremala na mama Mama Ntilie, baba yake na Genesis akawaambia watoke nje, kwa kuwa walikuwa na mazungumzo muhimu na Bwana na Bibi Rwegoshora!

Hiyo ilikuwa ishara ya kukataliwa! Genesis na Farida wakatoka kwa unyonge, huku Farida akilia kwa uchungu.
Je, nini kitatokea? SONGA NAYO...

HUZUNI ilikuwa ndani ya mioyo yao wote, Genesis alijua wazi kilichotokea. Ni kweli kwamba wazazi wake hawakuwa tayari kuona anakuwa na uhusiano na mtoto anayetoka kwenye familia ya kimasikini kama Farida! Aliwajua vizuri sana wazazi wake, siku zote walipenda kuwaheshimu na kuwathamini zaidi watu wenye majina yenye heshima!

Neno ‘Mama Lishe’ na Fundi Seremala’ yalitosha kabisa kumkosesha sifa Farida za kuingia katika nyumba ile ya thamani, iliyokuwa pembeni kabisa mwa Hoteli kubwa ya kifahari Golden Tulip.

Moyo wa Farida ulisononeka sana, alikuwa katika mateso makubwa ambayo ni kama aliyatarajia awali. Alitembea kwa huzuni huku Genesis akiwa nyuma yake, akizidi kumuonea huruma rafiki yake.

“Sio sababu lakini, siwezi kuishi bila Farida wangu!” Akawaza kichwani.
“Nampenda sasa nifanyeje?” Akazidi kuwaza.
Wakatoka hadi nje na kwenda kukaa kwenye viti vilivyokuwa kwenye bustani nzuri ya kupendeza. Uso wa Farida ulikuwa umechafuliwa kwa machozi.

“I need to go back home!” (Nataka kurudi nyumbani!) Farida alisema akitetemeka kwa woga.
“No! Farida...no...” (Hapana Farida...hapana...) Akajibu Genesis bila kuwa na maneno mengine ya kuendeleza mbele.

“I don’t have a reason to be here Genesis, remember your family is so reach and my family is poor, can you imagine that different?” (Sina sababu ya kuendelea kukaa hapa, kumbuka familia yako ni tajiri na sisi ni masikini, unaweza kuona hiyo tofauti?)

“It is not the reason, let me ask you a question!” (Siyo sababu, hebu nikuulize swali).
“Go on!” (Uliza!)
“Do you know what is inside my heart?” (Hivi unajua kilicho ndani ya moyo wangu).
“About what?” (Kuhusu?)

“Our relation!” (Uhusiano wetu)
“Yes, I know!” (Ndiyo, najua)
“You know what?” (Unajua nini?)
“We are friends!” (Sisi ni marafiki!)

“Only that?” (Hivyo tu!)
“Genesis mbona unanishangaza, kwani kuna nini kingine?” Farida akasema akiwa amemkazia macho, tena sasa akaamua kuzungumza kwa Kiswahili.

Walikuwa wanafunzi wa kidato cha pili, lakini tayari walikuwa na uwezo mzuri wa kuzungumza Kiingereza. Kwa viwango vya shule walizosoma, ilikuwa ni sahihi kabisa.

Farida alikuwa akijaribu kuuliza swali ambalo alikuwa na jibu lake kichwani, alijua ni kwa nini Genesis alimwuliza swali lile, jibu alikuwa nalo ndani ya moyo wake, kwamba wanapendana, lakini hakutaka kabisa kuonesha kwamba anajua jambo hilo.

Mila na desturi za Kiafrika zilimwongoza vizuri sana Farida, hakutaka kuonekana kama mwanamke ambaye kwao hakufunzwa vizuri.
“Farida, please, forgive me!” (Farida tafadhali naomba unisamehe) Baadaye Genesis akasema kwa sauti ya upole sana.

“For what?” (Kwanini?)
“For what happened, but I have a good message for you today!” (Kwa yaliyotokea, lakini nina ujumbe wako mzuri sana leo!)
“Just tell me!” (Niambie!)
“Farida, I love you!” (Nakupenda Farida!)

“Najua lakini tatizo ni kwamba familia yako hanikubali.”
“Usiseme hivyo tafadhali, unauumiza moyo wangu Farida, najua unafahamu kwamba nimetunza hili penzi kwa muda mrefu sana moyoni mwangu, leo ilikuwa siku ya kukuambia habari hizi, nataka kukuhakikishia kwamba, nakupenda sana na nitahakikisha nafanya kitu chochote kile ili niweze kuwa na wewe.

“Achana na wazazi wangu, hata wao hawakuchaguliwa wake wa kuwaoa, walikutana wenyewe na kuchaguana wenyewe, kwa hiyo hata sisi tunahaki zetu. Kama wana itikadi zao, hizo hazituhusu, tunatakiwa kuangalia mapenzi yetu,” Genesis alisema kwa utulivu akionekana kumaanisha kabisa alichokisema.

Tayari moyo wake ulikuwa umetapika nyongo ya mapenzi mazito aliyokuwa nayo dhidi ya Farida. Katika maisha yake yote hakuwahi kupenda kama alivyompenda msichana huyu ambaye mvuto wake haukuwa na mfano.

“Nimeshakuambia Genesis, naamini hata wewe unatambua kwamba nakupenda, lakini hapa tatizo ni wazazi. Hebu fikiria, kuniona tu, bila hata kujua kama tuna uhusiano au lah wamenichukia na kutuambia tutoke nje, vipi siku wakijua kwamba tuna uhusiano, si itakuwa balaa?”

“Hapana...nashukuru kwanza kwa kuniambia unanipenda, hilo ni jambo nililotarajia kutoka kwako. Kwa sasa tuishie kuwa tunapendana, hayo mambo mengine yatafuata baadaye.”
“Tutaona!”
“Jiamini mpenzi wangu!”

“Najiamini lakini tatizo...” Farida alitaka kuzungumza kitu lakini Genesis alishajua jambo alilotaka kuzungumza kwa hiyo akamkatisha mara moja.
“Sahau kuhusu wazazi wangu Farida, tuangalie mapenzi yetu!”
“Sawa, lakini naomba uniruhusu jambo moja.”

“Ni nini?”
“Naomba niondoke.”
“Subiri kidogo nakuja,” alisema Genesis na kuondoka bustanini.

Ilikuwa safari ya kumfuata dereva wao, baada ya kumuagiza awashe gari, alirudi haraka bustanini na kumuambia Farida asimame kwani muda wa kuondoka ulikuwa umefika. Wakaongozana moja kwa moja hadi kwenye gari, walipolifikia Genesis akafungua mlango wa nyuma.

“Hapana Genesis, nitatumia daladala usijali. Nitapanda hapa mpaka Posta, halafu huko nitachukua gari la Mbagala nitashuka nyumbani!”
“Hapana, twende na gari la nyumbani.”
“Hapana Genesis!”

“Kwanini? Kwanza ukumbuke kwamba ni gari hilihili ndilo lililokufuata nyumbani na kukuleta hapa, isitoshe, wewe ni mgeni wangu, natakiwa kuhakikisha umerudi nyumbani salama!”
“Hata daladala nitafika!”
“Sawa, lakini ujue kuwa sijafurahi!” Sauti ya Genesis ilisikika kavu, akiongea kwa upole kuliko kawaida.

Hiyo ilitosha kabisa kumfanya Farida agundue kwamba mpenzi wake alikuwa amekasirika. Ni jambo ambalo siku zote hakutaka kabisa litokee. Kwake ilikuwa bora Genesis akasirishwe na mtu mwingine, yeye awe mfariji wake. Akaingia kwenye gari.

“Ahsante sana!”
“Usijali mpenzi!”
Safari ikaanza. Tofauti na matarajio ya Farida, safari yao ilianzia Kariakoo, ambapo kwa mara nyingine tena Genesis alimwingiza madukani na kumchagulia nguo na viatu.

Farida akafurahi sana, baada ya hapo wakapanda kwenye gari na kwenda zao Mtoni Kwa Azizi Ally.
“Nashukuru sana Genesis, ahsante kwa kunijali na kunipa moyo!”

“Usijali mpenzi, ni jukumu langu kabisa kukufanya mwenye furaha, nawajua wazazi wangu, nitakuambia kitu cha wakati mwingine ili wakukubali!”
“Nitafurahi sana, maana najaribu kuyatafakari maisha bila wewe, nashindwa kabisa kuelewa yatakavyokuwa!”

“Bila shaka, hakuna kinachoshindikana mbele za Mungu, yeye anayejua vilivyomo mioyoni mwetu atatenda!”
“Amina.”
Wakaagana, Farida akaingia ndani kwao, Genesis akarudi kwenye gari. Dereva akawasha na kuondoka zao.
**
Muda wote walikuwa wakizungumza huku wakicheka, Dk. Rwegoshora alikuwa amepotezana kwa muda mrefu sana na Profesa Mshana. Furaha ikatawala katika sebule ile ya kisasa inayovutia.
“Hongera sana!” Dk. Rwegoshora hatimaye akasema.

“Ya nini?”
“Umejitahidi sana mzee mwenzangu. Unajua lazima uishi kwenye mazingira yanayofanana na hadhi yako! Kuna wenzetu wengine hawajui hilo, wanakuwa wagumu wa kufaidi maisha ipasavyo wakisahau hadhi zao! Hapa ni sehemu sahihi zaidi ya kuishi mtu kama wewe!”
“Ahsante sana Dokta, halafu tunaweza kuzungumza pembeni kidogo?” Profesa Mshana akasema.

“Bila shaka!”
“Jamani samahanini, nipo na mzee mwenzangu kule meeting room, tutarudi baadaye, lakini mama Genesis tafadhali mwambie msichana atuletee maji ya matunda!” Profesa Mshana alimwambia mkewe.

“Sawa darling!”
Muda huo huo wakasimama pamoja na kuanza kuongozana kwenda kwenye chumba cha mkutano. Macho yao yakapokelewa na chumba kizuri kilichopangwa masofa mazuri, chini kukiwa na zulia lenye manyoya laini kabisa. Wakaketi kwenye viti wakiendelea kuzungumza...

“Sasa umeshajipanga kuhusu shule atakayoendelea nayo mwanao?” Profesa Mshana akamwambia Dk. Rwegoshora.
“Hapana, vipi kuna shule nzuri unataka kunionesha nini?”
“Ndiyo, kama unavyojua mimi elimu kwanza, ndiyo msingi wa maisha ya wanangu. Kwanini usimpeleke St. Thomas?”

“Ipo wapi?”
“Morogoro, anasoma Genesis huko. Ni shule nzuri yenye maadili ya kidini, mtoto atakuwa kiakili na kiroho pia, patamfaa sana pale!”
“Kweli eh?!”

“Nakwambia ukweli, maendeleo ya mwanangu yananishawishi kwa kiasi kikubwa sana kukushauri na wewe umpeleke mwanao huko!”
“Sawa, naomba nilichukue hili wazo kama lilivyo, halafu nitazungumza na mama yake!”
“Hapana mzee mwenzangu, unadhani ni kwanini niliomba kuzungumza na wewe pembeni? Ni kwa sababu nilitaka tumalize hili jambo kama wanaume.”

“Ok! Nimekuelewa ndugu yangu, ushauri wako ni mzuri na wa maana sana, nitaufanyia kazi!”
“Tena kwa mafanikio makubwa!”
Wote wakacheka, muda mfupi baadaye wakasimama na kurejea sebuleni.

Ndani ya moyo wa Profesa Mshana kulikuwa na kitu kingine zaidi, alitamani sana kuunganisha familia yake na ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali! Alipenda sana watu wenye heshima kubwa!

Kikubwa alichowaza ni Genesis siku moja amuoe Bianca! Kuwasogeza shule ulikuwa mpango wa kwanza, ambao kwake yeye aliamini kuwa ungeweza kuwasogeza vijana hao na kuwa kitu kimoja. Wakiwa wanaingia sebuleni, Genesis akatokea mlangoni akiingia ndani, uso wake ukiwa umejaa makunyanzi!
Hasira yake ilisomeka wazi kabisa!
**
“Hizi nguo mpya umepata wapi? Na hiyo tabia umeanza lini? Kwanini unataka kutuingiza kwenye matatizo wewe mtoto?” Alikuwa ni mama yake Farida, akimwuliza mwanaye alipoingia ndani, muda mfupi baada ya kuachana na Genesis.

Farida hakuwa na jibu, alinyamaza kimya akiwa anatetemeka.
Je, nini kitatokea?

Comments

Popular posts from this blog

AirPods Fake Vs Real – How To Spot Fake AirPods In 2021 (Ultimate Guide)

AirPods Fake Vs Real – How To Spot Fake AirPods In 2021 (Ultimate Guide) Need your item authenticated by us? Proven expertise, not self-claimed. Get checked by the industry's top experts. Get Authenticated Want this item? Buy it from our partners! Looking to learn how to spot fake AirPods? Scared of getting scammed? Look no further, as we’ve compiled the most complete legit check guide for Apple AirPods. To put it shortly, the quickest way to spot fake AirPods is to scan the serial number found on the inside of the case (see pictures below on how to find that serial number). Once you get that code, pop it through  checkcoverage.apple.com  and see whether Apple confirms it for you. If you can’t get ahold of this code, we’ve added fake vs real comparisons for the actual AirPods below! Remember, fake AirPods will always compromise on quality. To highlight the most common places where these compromises are made, we’ve put together the comparisons you’ll find below. In this gu...

Breaking news: Haji S. Manara ahamia yanga

  Aliekua msemaji mkuu wa Simba SC maarufu H. S. Manara. Baada ya kutokea kutokuelewana na klabu yake aliyokua akiitumikia, leo tar 24 August 2021 ametambulishwa rasmi Yanga SC na ya kusaini kandarasi akiwa kama msemaji huru.  Nimekiwekea baadhi ya matukio bofya kuangalia. Tujikumbushe pia enzi akiwa Simba SC. 

Aina ya sita ya vyakula ambavyo vikichanganywa hugeuka sumu

  Aina ya sita ya vyakula ambavyo vikichanganywa hugeuka sumu Kila binadamu ana kile alichojaaliwa na Mungu. Siku zote anachoamua mmoja kula huenda kikawa sumu kwa mwingine. Chakula anachokula mtu kinaenda sanjari na hali ya kiafya. Wengine huumwa hadi kusababisha kupoteza uhai na hii ni baada tu ya kupendelea kuchanganya chakula. Mtu mmoja anaweza kula sawa na kwa urahisi, ila kwa mwingine kikageuka sumu. Hali hii huchochewa zaidi na matokeo ya baadae pale unaposhindwa kuweka mchanganyiko sahihi na wenye afya zaidi . Kila aina chakula ina faida zake, ila kinapochanganywa kinaweza kusababisha shida kwa mtu. Kwa watu ambao wanataka kuchanganya lishe ili kupunguza unene na vichocheo vyake ni vyema kushauriana na wataalamu jinsi ya kupanga lishe bora. Mtaalam wa lishe wa Nigeria Habiba Haruna ameiambia BBC kuhusu aina sita za chakula ambazo zinaweza kuwa sumu kwa mtu yeyote. Samaki na Maziwa Samaki na Maziwa ni vyakula vyenye virutubisho lukuki na kuvichanganya katika sehemu moja vina...