Wananchi watalazimika kulipa Sh20,000 kila mmoja wakati wa kuhuisha Vitambulisho vya Taifa, tofauti na siku za nyuma vilipotolewa bila malipo. Kundi la kwanza la Vitambulisho vya Taifa ambavyo vilitolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) mwaka 2013 vinatarajiwa kumalizika muda wake kuanzia mwaka ujao (2023) Hata hivyo mamlaka hiyo imetoa tamko la kuwaondolea wasiwasi ikisema kwa sasa imeharakisha utengenezaji wa vitambulisho. “Tunaogopa kwa sababu kuna wenzetu hapa mtaani tangu wajiandikishe, huu ni mwaka wa pili hawajapata vitambulisho, walichonacho ni namba tu." Alisema mkazi mmoja wa jijini Dar Es Salaam baada ya mahojiano ya mda mfupi kuhusu tathmini zoezi la vitambulisho vya taifa. Serikali imewahi kusema mara kadhaa kuwa kuna vitambulisho kadhaa vimetelekezwa katika ofisi za Nida. " Isitoshe sisi ambao tutataka ku-renew wasipobadilika nadhani tutapata tabu sana muda ukifika tutaendelea kutumia namba badala ya kitambulisho ,” aliongeza. Vitambulisho vya Taifa ...