Kuanzia Februari 1, 2022 matumizi ya daraja hili yataanza rasmi, hii ni kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo tar 30 Jan 2022.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa leo January 30 2022 ametangaza rasmi kukamilika kwa 100% kwa daraja la Tanzanite ambalo limejengwa juu ya bahari kutoka maeneo ya Aga Khan mpaka Osterbay Dar es salaam na sasa magari yataanza kupita rasmi kuanzia February 1 2022.
Baada ya kufanya ukaguzi leo, Waziri Mbarawa amesema daraja hili lililogharimu zaidi ya Bilioni 240 litakua likitumika bure kwa Wananchi wote.
Comments
Post a Comment